Javier Zanetti anasema Inter wana imani kubwa na kocha wao Simone Inzaghi na wanaamini wanaweza kuweka changamoto kubwa kutwaa tena taji la Serie A .

 

Zanetti: Inter Haijawahi Kumtilia Shaka Inzaghi

 

Intermilan walinyang’anywa taji hilo na wapinzani wao AC Milan katika msimu wa kwanza wa Inzaghi baada ya kuvutiwa na kocha mkuu kutoka Lazio kwa mkataba wa miaka miwili . Inter wapo nafasi ya 7 baada ya kupokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Udinese katika mchezo wao wa mwisho kabla ya mapumziko ya Kimataifa.

Hicho kilikuwa kipigo chao cha tatu Serie A katika mechi saba msimu huu na pia walichapwa 2-0 na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa huko San Siro. Makamu wa Inter Zanetti anasema uongoza haujawahi kuwa na shaka yoyote kwamba Inzaghi ndiye mtu sahihi klabuni hiyo.

 

Zanetti: Inter Haijawahi Kumtilia Shaka Inzaghi

Aliiambia Tuttomercatoweb.Com: “Siku zote tumekuwa na imani na Inzaghi, sifa sio za mtu mmoja tuu.”Kuna kundi ambalo lina malengo ya wazi kabisa na sote tuanelekea katika mwelekeo mmoja”.

Nahodha huyo wa zamani wa Argentina Zanetti, anatarajia Inter kuwa na nguvu msimu huu licha ya kuanza vibaya. Aliongeza: “Lazima tuwe timu yenye uthabiti, unyenyekevu, na na hapo iatategemea uwezo wetu wa kuwa wahusika wakuu kwasababu nina uhakika kwamba kuna masharti ya kufanya hivyo”

 

Zanetti: Inter Haijawahi Kumtilia Shaka Inzaghi

Inter watarejea dimbani mechi ijayo ya Serie A dhidi ya Roma Jumamosi Ijayo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa