Katika Dimba la Anfield jioni ya leo kutapigwa bonge mechi kati ya magwiji wa zamani wa vilabu pendwa zaidi nchini Uingereza vilabu vya Liverpool na Manchester United wenyewe wakiuita mchezo wa magwiji wa kaskazini.

Magwiji wa kaskazini ni jina la mchezo utakaokwenda kupigwa jioni ya leo katika dimba la Anfield ikimbukwe Manchester United na Liverpool ni vilabu vinavyotokea kaskazini mwa nchi ya Uingereza, Na ndio sababu mchezo kati yao huitwa dabi ya kaskazini pamoja na kua timu hizi hazitoki jiji moja huku ikiaminika ndio timu mahasimu zaidi nchini humo kuanzia ukongwe mpaka mataji.

anfieldVilabu hivyo ambavyo ndio vinaongoza kwa mataji nchini Uingereza hucheza mechi hizi za magwiji wa zamani wa klabu kwasababu ya kutaka kurudisha kwa jamii kupitia mapato yanayopatikana katika mechi hizo.

Miongoni mwa magwiji watakaoshiriki mchezo huo jioni ya leo kwa upande wa united kuna magwiji kama Roy keane,Dimitar Berbatov,Michael Carrick,Darren Fletcher,pamoja Wes Brown kwa upande wa Liverpool miongoni mwa magwiji watakaokuepo pia ni kama Jersey Dudek,Xabi Alonso,Martin Skrtel,Albert Riera, pamoja na Stewart Downing.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa