Klabu ya Yanga inatarajia kumualika Polisi Tanzania hapo kesho majira ya saa 1:00 usiku katika mchezo wao wa ligi kuu ya NBC.

 

Yanga Kukiwasha Dhidi ya Polisi Tanzania Kesho

Young Africans ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi msimu uliopita na wapo kileleni mpaka sasa wakiwa wamejikusanyia pointi 38 kibindoni, huku wakiwa na matumaini ya kutetea taji hilo msimu huu tena.

Polisi Tanzania wao bado wana hali mbaya kwani ndio vibonde wa ligi hadi sasa wakiwa nafasi ya 16, baada ya kucheza michezo michezo yao 15, ushindi mara mbili, sare tatu na kupoteza mara 10 hadi sasa pointi zake 9.

Yanga Kukiwasha Dhidi ya Polisi Tanzania Kesho

Wakati Wananchi wameshinda michezo 12 kati ya 15 walizocheza, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja tuu hadi sasa.

Katika mechi tano za mwisho walizokutana Yanga ameshinda nne, wakatoa sare moja wakati kwa upande wa Polisi ambao wana kocha mpya Mwinyi Zahera wakiwa hawajapata ushindi wowote.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa