"Yanga ni dhaifu": Kocha Kurugenzi FC

UNAWEZA ukashangaa kama utasikia kauli ya kocha ambaye timu yake ilipokea kichapo cha mabao kutoka kwa Yanga 8-0, akasema mpinzani wake ni dhaifu na hiyo imetokea kwa kocha wa Kurugenzi FC.

Kurugenzi FC, ilipokea kichapo cha mabao 8-0 kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa Azam Sports Federation uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa. Kocha huyo, Bernad Magogo alisema bila uoga kuwa timu hiyo ni dhaifu.

Yanga ni dhaifu": Kocha Kurugenzi FC

Magogo alisema: “Wachezaji wangu walifungwa kwa makosa madogo madogo, ila Yanga ni dhaifu, kwenye eneo lao la ulinzi siyo imara, kama inatokea timu inacheza kwa nguvu inaweza kupata mabao”.

“Walicheza kwa makosa sana kwenye eneo lao la ulinzi, kulikuwa na udhaifu Fulani hivi. Bahati mbaya wachezaji wangu bado ni wachanga na walikutana na wachezaji bora zaidi.”

Acha ujumbe