Mabingwa Watetezi Yanga Kuanza Leo Dhidi ya Kurugenzi FC

Klabu ya Yanga ambao ndio mabingwa wa Kombe hili la Shirikisho ambalo linaendelea leo hii watakuwa Dimbani kwa Benjamin Mkapa kukiwasha dhidi ya Kurugenzi FC ya mkoani Simiyu.

 

Mabingwa Watetezi Yanga Kuanza Leo Dhidi ya Kurugenzi FC

Mchezo huo wa Mabingwa hao unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku huku michezo mingine ikiwa imekwishaanza na baadhi ya timu kushinda ushindi mkubwa kwa kupachika mabao mengi.

Yanga walitwaa taji hilo kutoka kwa Coastal union baada ya kwenda dakika 120, hivyo leo hii wanatarajiwa kuanza kutetea taji lao dhidi ya timu hiyo ya daraja la pili.

Mabingwa Watetezi Yanga Kuanza Leo Dhidi ya Kurugenzi FC

Azam na Ihefu wao wameshinda mabao 9 katika mechi zao za kwanza huku Simba yeye akishinda mabao 8 katika mchezo wake hapo jana, sasa ni zamu ya Young Africans watashinda ngapi?

Acha ujumbe