Yanga: Azizi KI ni Mkali wa Hizi Kazi kabisa

KWA mzunguko wa kwanza majukumu ya mipira iliyokufa ndani ya kikosi cha Yanga yalikuwa kwenye miguu ya Aziz KI.

Nyota huyu bado hajaonyesha makeke yake kama ilivyokuwa ndani ya ASEC Mimosas lakini taratibu anazidi kuimarika.

Ni mabao mawili ametupia ndani ya ligi msimu huu wa 2022/23 ndani ya kikosi chake kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Yanga: Azizi Ki ni Mkali wa Hizi Kazi kabisa

Alikuwa ni miongoni mwa walioanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC.

Wakati ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukisoma Namungo 0-2 Yanga alikuwa sababu ya bao la Namungo kwa pigo lake la faulo iliyomshinda kipa Jonathan Nahimana na kukutana na Yannick Bangala dakika ya 40.

Yanga: Azizi Ki ni Mkali wa Hizi Kazi kabisa

Pia bao moja kati ya mawili amefunga kwa pigo la faulo ilikuwa dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa, dakika ya 45 alipomtungua Aishi Manula.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa Aziz ni mchezaji mzuri lakini anahitaji muda kuzidi kuimarika.

Acha ujumbe