Kocha wa klabu ya As roma raia wa Ureno Jose Mourinho inaelezwa shirikisho la soka nchini humo lina mpango wa kumkabidhi timu ya taifa ya Ureno kama mrithiwa kocha wasasa Fernando Santos.

Timu ya taifa ya Ureno imetupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia kwenye hatua ya Robo fainali na timu ya taifa ya Morocco, Huku wadau wengi wakiona kama kocha wasasa wa timu hiyo Fernando Santos muda wake umepita na ni muda wa kuachia ngazi kwenye timu hiyo na aje kocha mwingine.jose mourinhoInaelezwa shirikisho la soka nchini Ureno limepanga kumpa timu kocha Jose Mourinho ambaye ni kocha aliyepata mafanikio makubwa sana kwenye ngazi ya klabu akishinda kila taji ambalo amegombania. Hivo shirikisho hilo linamuona kama mtu sahihi wa kuvaa viatu vya kocha Fernando Santos.

Taarifa zaidi zinaeleza kua halitampa pingamizi kocha Jose Mourinho kuendelea na majukumu yake kwenye klabu yake As Roma, Hivo kocha huyo ataruhisiwa kuendelea na majukumu yake kwenye klabu yake huku akifundisha timu ya taifa ya Ureno.jose mourinhoKocha Santos inaelezwa atatangaza kuachia ngazi katika timu ya taifa ya Ureno muda wowote kuanzia sasa, Licha ys kutolewa kwenye kombe la dunia kocha huyo atakumbukwa zaidi nchini humo baada ya kuisaidia timu hiyo kubeba taji la Euro mwaka 2016 na taji la Uefa Nations League mwaka 2019.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa