LICHA ya kuwa ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, mwanadada Barbara Gonzalez ataendelea kusalia ndani ya kiti hicho kwa mwezi mmoja zaidi.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally ambaye aliweka wazi kuwa Uongozi wa juu ulishapitisha na kukubali uamuzi wake wa kujiuzulu lakini hataondoka hadi akamilishe baadhi ya majukumu.

Ahmed alisema kuwa Barbara ataondoka mara tu baada ya kumaliza kusimamia masuala ya usajili wadirisha dogo na mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kumbe Barbara bado yupo yupo Simba

“Ni kweli C.E.O wetu  aliandika barua ya kujiuzulu kwenye nafasi yake na Uongozi ulibariki maamuzi hayo. Lakini bado atasalia kwenye klabu hiyo mpaka akamilishe baadhi ya majukumu.

“Anatakiwa asimamie kwanza usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa Desemba 15, lakini pia hadi asimamie mchakato wa uchaguzi wa klabu yetu,” alisema Ahmed.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa