Golikipa wa timu ya taifa ya Ufaransa Hugo Lloris amesema mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uingereza atarudi akiwa na nguvu zaidi baada ya kukosa penati katika mchezo wa robo fainali wa kombe la dunia dhidi ya Ufaransa.
Harry Kane alikosa penati katika mchezo wa Robo fainali wa kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa ambapo staa huyo alikua anakabiliana na mchezaji mwenzake wa klabu ya Tottenham Hugo Lloris ambaye alikua golikipa wa Ufaransa.Harry Kane ambaye alikua ana nafasi ya kuweza kufufua matumaini ya Waingereza kupitia penati hiyo aliyokosa kwani walikua nyuma kwa mabao mawili kwa moja, Lakini Kane alishindwa kusawazisha na kukosa penati na mchezo huo kumalizika kwa Uingereza kupoteza kwa mabao mawili kwa moja.
Golikipa Hugo Lloris amesema anaamini Kane atarudi kua sawa tu katika klabu yake ya Tottenham na timu ya taifa ya Uingereza huku akisema wachezaji wengi wakubwa wamewahi kukosa penati muhimu kama Ronaldo, Mbappe,na Messi hivo sio jambo geni sana na mchezaji huyo atakua sawa tu.Harry Kane ambaye alikua ,fungaji bora wa michuano ya kombe la dunia iliyopita mwaka 2018 lakini mwaka huu ameshindwa kumaliza juu kwenye ufungaji wa mabao akiwa na mabao 3 na kushuhudia timu yake ikitupwa nje ya michuano kwenye hatua ya robo fainali.