Busquets Atangaza Kustaafu Hispania

Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Sergio Busquets ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania baada ya kuitumia kwa muda mrefu.

Kiungo huyo amefanya maamuzi hayo wiki kadhaa baada ya timu ya taifa ya Hispania kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia kwenye hatua ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Morocco.busquetsKiungo huyo ambaye anatajwa kama kiungo bora wa ulinzi kwa muongo mmoja uliopita baada ya kucheza kwa mafaniko makubwa na kiwango bora sana kwenye klabu yake ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania.

Kiungo Sergio Busquets anaondoka timu ya taifa ya Hispania baada ya kuitumikia nchi hiyo kwa takribani miaka 15 na kucheza michezo 143 na timu hiyo huku akifanikiwa kushinda mataji mawili makubwa na taifa hilo ikiwemo taji la kombe la dunia mwaka 2010 na kombe la ulaya Euro mwaka 2012.busquetsKiungo Busquets ametangaza kustaafu timu ya taifa ya Hispania leo na kuandika kwenye mitandao yake ya kijamii , Huku akishukuru wachezaji wenzake, makocha wote na uongozi ambao ameshirikiana nao kwa kipindi chote ambacho amekua akitumikia nchiyo kwa mafanikio makubwa.

Acha ujumbe