Simba Wakifanya Haya Pre Season Kitawaka, Ubingwa Kubeba

Viongozi wa Simba wanapambana sana kurudisha heshima ya klabu hiyo na kuijenga timu upya lakini pia kurudisha Imani ya mashabiki na wanachama wa simba. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Lakini kabla ya kwenda Pre season kuanza Mnyama anatakiwa kuhakikisha mambo yafuatayo yanakamilika;

1. Kumaliza kuagana na wachezaji ambao wao viongozi wameona inafaa waondoke. Hili liwe kabla ya preseason kuanza ambapo hadi sasa zimetoka Thank You nne tu, ya John Bocco, Saidoo, Chilunda na Kennedy Juma.

2. kumaliza usajili mpya kwa nafasi ambazo wao wanaona zinafaa kusajili. Hili liwe kabla ya Pre season kuanza Kwasababu itakuwa mbaya wachezaji wapya Kuja baada ya Pre season kuanza itaathiri ujenzi wa timu, yatajirudia ya msimu uliopita wachezaji wengine wanakuja kugundulika wana majeraha ya muda mrefu, timu inaingia gharama ya kuvunja mikataba na inakuwa imepoteza muda.

3. kuhakikisha benchi la ufundi liko vizuri na limekamilika kwa maana ya kupata makocha wenye uwezo mkubwa sana kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya (Pre season). Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

4. kuhakikisha Kwa level ya uongozi Kuna utulivu Kwa kufanya vikao vyote vya umuhimu na kumaliza tofauti zilizopo kati ya upande wa 51% na 49% ili tutengenezee organization nzuri.

5. kuhakikisha pia ushiriki wa mashabiki (fans engagement) inarudi vizuri hii itawasaidi hata kujiandaa na tamasha kubwa la Simba Day haitakuwa ngumu kuwaita mashabiki. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Acha ujumbe