Crescentius Magori Afunguka A-Z Usajili wa Lameck Lawi Simba

Crescentios Magori ametolea ufafanuzi wa suala la usajili wa beki wa kati kutoka Coastal Union Lameck Lawi, ambapo inasemekana Simba ilikiuka makubaliano ya namna ya kumsajili mchezaji huyo. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Magori amezungumzia suala hilo kwa undani wake huku akisema kwamba, ni kweli walilipa pesa nusu lakini baadae walimalizia zilizobaki.

Magori aliyasema hayo kupitia Chombo cha Habari cha EFM, na kubainisha kwamba, walikubaliana kabla ya chezaji huyo kusajiliwa SIMBA waliwataka Coastal Union wamruhusu kwanza mchezjai huuyo afanyiwe vipimo vya afya.

“Katika hali ya kawaida hatukutegemea hili litokee, kwakuwa limetokea itabidi tukabiliane nalo, lakini mchezaji huyo amesajiliwa na Simba SC na kila kitu kipo tayari”

“Hata hiyo klabu inayomtaka (ya Nje), waambie hatutaishitaki Coastal Uniion pekee tutawashitaki wote”

Magori aliendelea kwa kusema haya;

“Ndio tulichelewa kumaliza kulipa pesa, tulilipa nusu lakini mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yoye ya usajili”

“Tumemsajili Lameck Lawi kwa kufuata utaratibu tunafanya kazi kwa uweledi, hoja zao ni dhaifu kusema mkataba umevunjika kwa sababu pesa haikulipwa yote”

“Wangesema mapema kama ukichelewa kulipa mkataba unavunjika. Mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yote na nyaraka zote tunazo hata tukienda FIFA. Mpira ni FIFA hauishii hapa”

“Kilichotokea Coastal Union wakapata deal kutoka nje ndio maana wakabadili maamuz. Kiukweli hili limetusumbua sana na tuko tayari kukabiliana nalo”

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe