AHMED ALLY AANZA KUTAMBA MAPEMA

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa Kwa mipango yao ya usajili waliyopanga, basi nchi itasimama watakapoanza kitambulisha.

Akizungumza na Meridian Sports Ahmed alisema hawatakuwa na muda wa kufanya makosa tena, kwani kilichowatokea kwenye misimu mitatu mfululizo kimewapa funzo kubwa.AHMED ALLY“Tumeteseka vya kutosha, misimu mitatu ya kukosa Ubingwa umetupa funzo kubwa mno, mipango ya usajili tuliyopanga nchi hii itatikisika.

“Msimu ujao wa mashindano 2024-25 kuna watu watakufa kutokana na wasiwasi wa maisha kwa ambacho watakifanya kwa mashabiki zao ambao wamekuwa na kiu ya kuona ubora wa timu hiyo unarejea,” alisema Ahmed Ally.

Acha ujumbe