INAELEZWA kuwa, kiungo mshambuliaji wa Rayon Sports, Leandre Essomba Willy Onana ambaye raia wa Cameroon, amekuja ar es Salaam kwa siri kwa ajili ya kufanikisha dili la kujiunga na Simba. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, msimu huu alimaliza akiwa kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Rwanda akifunga mabao 16.
Willy Onana ni kati ya wachezaji wanaotajwa katika usajili wa Simba kuelekea msimu ujao ambao utaanza kufanyika mara dirisha kubwa kufunguliwa hivi karibuni. Ukiwa na meridianbet unapata odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.
Mmoja wa mabosi wa Simba, alisema kuwa, kiungo huyo ametua nchini na kufichwa katika moja ya hoteli kubwa kwa ajili ya kufanya mazungumzo sambamba na kusaini mkataba.
Bosi huyo alisema mazungumzo hayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika baada ya mchezaji mwenyewe kufikia muafaka mzuri wa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Aliongeza kuwa, kiungo huyo amekubali kusaini mkataba huo wa miaka miwili baada ya ofa nzuri ambayo amewekewa mezani ili kukamilisha dili hilo.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
“Muda wowote Onana atasaini Simba sambamba na kutambulishwa mara baada ya dili hilo kukamilika kwa asilimia kubwa huku mkataba wake ukiandaliwa kwa ajili ya kusaini.
“Huenda akawa mchezaji wa kwanza mpya kusajiliwa na Simba, na uzuri ni kwamba kocha mwenyewe anafahamu uwezo wa kiungo huyo ambaye amekuwa mfungaji bora wa ligi msimu huu.
“Onana yeye mwenyewe ameonesha nia kubwa ya kuichezea Simba ambayo anaamini itamtangaza kimataifa msimu ujao, wakati tukienda kucheza michuano ya kimataifa,” alisema bosi huyo.
Akizungumzia hilo la usajili, Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Wachezaji wengi wakubwa wanataka kuja kuichezea Simba, hiyo ni kutokana na ukubwa wa timu yetu.
“Ipo fedha ya kusajili mchezaji yeyote atakayehitajika na benchi la ufundi, yupo mwekezaji wetu Mo (Mohammed Dewji) ambaye ameweka pesa nyingi kwa ajili ya kufanya usajili.”
Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.


