Nabi Kutimka Jangwani Muda Wowote

Kocha wa klabu ya Yanga Nassredine Nabi taarifa zinaeleza kua kocha huyo raia wa kimataifa wa Tunisia atatimka ndani ya klabu hiyo muda wowote kuanzia sasa.

Kocha Nabi inaelezwa ameshawaeleza viongozi wa klabu ya Yanga nia yake ya kutimka ndani ya timu hiyo baada ya kumalizika tu kwa fainali ya kombe la Shrikisho nchini Algeria, Hivo ni wazi kocha huyo atatimka ndani ya timu hiyo baada ya mkataba wake kumalzika.NabiKocha huyo amamemaliza mkataba wake ndani ya Yanga ambapo aliongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya timu hiyo mwaka jana na sasa umemalizika, Inaelezwa kocha huyo anaelekea Afrika Kusini kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini humo.

Kocha Nabi amefanikiwa kukaa nchini Tanzania kwa miaka miwili na nusu akiitumikia klabu ya Yanga akifanikiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya timu hiyo, Kwani ametwaa mataji mawili ya ligi kuu, mataji mawili ya kombe la Azam, Ngao ya jamii mara mbili na kubwa kabisa kuifikisha klabu hiyo fainali ya kombe la Caf shirikisho.NabiNassridine Nabi anaondoka jangwani akiwa na heshima kubwa kama kocha ambaye ameipa historia kubwa klabu hiyo, Kwani amefanya jambo ambalo halijawahi kufanyika ndani ya klabu hiyo japo anaondoka kipindi wanajangwani wakiwa wanamuhitaji sana.

Acha ujumbe