Arsenal Yamgeukia Havertz

Klabu ya Arsenal inafanya mazungumzo na mchezaji wa Chelsea raia wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz kwajili ya kumsajili katika dirisha hili kubwa.

Arsenal wanataka kuwasilisha ofa kwa klabu ya Chelsea kwajili ya kumnunua kiungo huyo wa kijerumani Kai Havertz ambaye amekua hana msimu mzuri hivi karibuni na mchezaji mwenyewe anataka kuondoka ndani ya timu hiyo.ArsenalWashika mitutu wa London wanataka kuwasilisha dau mezani kwajili ya Havertz pamoja na kiungo wa klabu ya West ham United ambaye wamekua wakimfukuzia kwa muda mrefu Declan Rice ili kuboresha timu yao kuelekea msimu ujao.

Kai Havertz alikua akihitajika na klabu ya Real Madrid lakini mpaka sasa inaonekana wababe hao wa soka nchini Hispania wamejitoa katika mbio hizo, Huku Arsenal sasa wakiuonesha nia ya dhati ya kumchukua kiungo huyo.ArsenalArsenal wanataka kuboresha timu yao zaidi baada ya kua na msimu mzuri mwaka 2022/23 licha ya kukosa ubingwa wakiamini kama wataboresha timu yao basi wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao na hata kubeba ubingwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.