Rashford Achukizwa na Ubingwa wa City

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Marcus Rashford amekiri kutokufurahishwa na ubingwa wa klabu ya Manchester City ambao ni majirani zao katika jiji la Manchester.

Kauli hiyo ya Rashford imekuja baada ya klabu ya Manchester City kufanikiwa kutwaa mataji matatu katika msimu mmoja na kufikia rekodi ya Manchester United ya mwaka 1999 ambayop imedumu kwa takribani miaka 24.RashfordMshambuliaji huyo amezungumza na waandishi wa habari wakati akiwa na timu ya taifa ya Uingereza na kusema hajapendezwa na majirani zao walichokifanya, Lakini akasema ndio mpira ulivyo na kuongeza haimvunji moyo bali imewapa nguvu kama timu ili kuweza kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

Mshambuliaji Rashford ambaye amekua na msimu bora sana ndani ya klabu hiyo akifanikiwa kufunga mabao 30 ndani ya klabu ya Manchester United ameahidi mafanikio ya Man City waliyoyapa msimu huu yatawapa nguvu ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao.RashfordMarcus Rashford anaamini Manchester United inaweza kufanya vizuri zaidi msimu ujao kutokana na kuona mafanikio ya majirani zao waliyoyapata ndani ya msimu huu, Kwakua ni kitu ambacho wanakitamani kitokee kwa upande wao pia.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.