Klabu ya Simba imeanza safari yao mapema leo kuelekea nchini Morocco kucheza mchezo wao wa mwisho wa makundi wa kombe la klabu bingwa barani Afrika utakaopigwa siku ya Ijumaa dhisdi ya Raja Casablanca.
Klabu ya Simba itakwenda kukamilisha ratiba kwenye mchezo huo kwani tayari klabu hiyo imeshafuzu hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, Lakini klabu ya Wekundu wa Msimbazi wanataka kwenda kuweka heshima Morocco kwani mchezo huo hawauchukulii lelemama.
Wekundu hao wa Msimbazi wamekua kwenye kilele cha mafanikio kwa michuano ya Afrika kwa timu zinazotoka nchini Tanzania kwani kwenye miaka sita ndio klabu pekee iliyofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Afrika mara nne ikionesha namna gani timu hiyo inafanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Simba ilipokea kichapo ha mabao matatu kwa bila katika uwanja wao wa nyumbani wa Benjamin Mkapa na kuvunja rekodi ya klabu hiyo katika uwanja huo, Lakini klabu hiyo ilijikwamua na kuweza kuvuna alama tisa na kuweza kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Klabu ya Simba inakwenda Morocco kuhakikisha inacheza mchezo wake wa mwisho kama kipimo kuelekea michezo mingine ya mbele, Beki wa klabu hiyo Shomari Kapombe alieleza kua licha ya kufuzu tayari lakini wanakwenda kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa na kuuchukulia kama kipimo cha michezo yao inayofuata hivo hawatauchukulia kiuwepesi.

