Simba Yamfukuzia Adebayor

Klabu ya Simba inamfukuzia kwa karibu mshambuliaji wa kimataifa wa Niger Victorien Adebayor ambaye anakipiga klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco.

Simba wameonesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo kabla hata hajajiunga na klabu ya klabu ya RS Berkane, Lakini wekundu hao wa msimbazi walizidiwa kete na wababe hao kutoka nchini Morocco lakini wamerudi tena katika vita ya kumuwania mchezaji huyo.simbaMchezaji Victorien Adebayor ameonesha nia ya kutaka kujiunga na klabu ya Simba mpaka sasa, Kwani klabu ya RS Berkane hapati nafasi ya kucheza zaidi hivo anatamani zaidi kukipiga ndani ya viunga vya Msimbazi.

Klabu ya Simba mpaka sasa inatakiwa kufanya mazungumzo na klabu ya RS Berkane ambayo bado ina mkataba na mchezaji huyo, Hivo wababe hao wa soka Tanzania wanatakiwa kukaa mezani na Berkane kwajili ya kumpata mchezaji huyo.simbaTaarifa zinaeleza kua mchezaji Adebayor amewasha taa ya kijani kwa wekundu wa msimbazi kwa kuonesha yuko tayari kuwatumikia, Lakini mtihani kwa klabu hiyo kutoka mitaa ya Kariakoo jijini Dar-es-salaam wanatakiwa kutoa kiasi ambacho Berkane watahitaji.

Acha ujumbe