Tanzania Yafufua Matumaini Afcon

Timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars imefufua upya matumaini ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2024 baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao bao moja kwa bila leo dhidi ya Niger.

Timu ya taifa ya Tanzania imepata ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Niger leo katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa Benjamin Mkapa, Huku bao pekee lililowapa Tanzania alama tatu likifungwa na Simon Msuva mnamo dakika ya 69 ya mchezo.TanzaniaTaifa Stars baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa leo imefanikiwa kufikisha alama 7 na kushika nafasi ya pili kwenye kundi F ambapo mpaka sasa wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Algeria ugenini.

Tanzania kama itafanikiwa kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Algeria na Uganda wakatoka sare leo dhidi ya Algeria au kufungwa basi watakua wamefuzu, Lakini kama Uganda watashinda leo mtanange utakua bado ni mgumu mpaka mchezo wa mwisho ndio utaamua zaidi.TanzaniaDua nyingi za Watanzania zinaelekea katika mchezo kati ya Uganda ambao wapo nyumbani dhidi ya Algeria na kuomba wafungwe ili Kutengeneza mazingira mepesi kwa Tanzania kufuzu katika mchezo wa mwisho, Kwani Uganda wakifungwa leo Taifa Stars itahitaji sare tu mchezo wa mwisho ili kufuzu Afcon 2024.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.