Klabu ya Simba SC imetinga hatua ya robo fainali kibabe sana baada ya kuitwanga Horoya kwa mabao 7-0 na kuweka historia ya kuwa timu mojawapo ambayo imetoa kipondo kikali kwenye klabu bingwa hatua ya makundi.
Vipondo vingine vilifanywa na Raja Casbalanca mwaka 1998 baada ya kutungua Yanga mabao 6-0, Kipondo kikingine alipigwa CR Belouzidad cha mabao 7-0 dhidi ya Asec Mimos 2001, na kipondo kingine kilitokea mwaka 2019 cha ambapo TP Mazembe alimfunga Club Africain mabao 8-0, na kingine ni hiki cha Simba kwa Horoya.
Mabao hayo ya kuizamisha Horoya yalifungwa na Cloutus Chama akitupia Hat trick, Baleke mawili, Kanoute mawili na kuwafanya kupata pointi 09 kwenye msimamo wa ligi huku Raja Casablanca akiwa bado kinara.
Mechi ya mwisho kwenye hatua hii ya makundi Mnyama atacheza dhidi ya Raja huku kila timu ikiwa tayari imeshafuzu.