SINGIDA BLACK STARS WANA KIPA LA MPIRA

KIPA wa mpira Mohammed Kamara anatarajia kuwasili nchini leo Julai 10 2024 kwa ajili ya kukamilisha dili la kujiunga na Klabu ya Singida Black Stars ambayo inashiriki Ligi Kuu Bara.

Mbali na kushiriki Ligi Kuu Bara Singida inashiriki mashindano ya Kagame na Julai 9 2024 ilikuwa uwanjani kusaka ushindi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex dhidi ya APR.

Ni Metacha Mnata ambaye ni ingizo jipya ndani ya timu hiyo akitokea Yanga alianza langoni kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Mwamba huyo anatoka Sierra Leone atakuwa mlinda mlango namba moja wa kikosi timu hiyo inayonolewa na Patrick Aussems maarufu kama Uchebe.

Uchebe aliweka wazi kuwa wanatumia mashindano hayo kuwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kuelekea kwenye msimu mpya wa 2024/25.

“Tunatambua kwamba mashindano haya yana ushindani mkubwa, kikubwa tutayatamia kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ambao utakuwa na ushindani mkubwa.”

Acha ujumbe