Tanzania Yaifunga Uganda

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imefanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Uganda The Cranes bao moja kwa bila katika mchezo wa kutafuta tikiti ya michuano ya matifa barani Afrika mwakani.

Timu ya taifa ya Tanzania ilionekana kuutaka mchezo kuanzia kipindi kwani ilionesha kufanya mashambulizi ya hapa na pale huku ikimiliki mpira kuzidi wenyeji wa mchezo huo timu ya taifa ya Uganda, Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikua hazijafungana.TanzaniaKipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu zote zikionekana kuhitaji alama tatu muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri, Dakika ya 68 ya mchezo winga matata Simon Msuva alimalizia krosi safi iliyopigwa na Dickson Job na kuipatia Taifa stars bao la kuongoza katika mtanange huo.

Baada ya Tanzania kupata bao la kuongoza kupitia kwa Simon Msuva waliendelea kushambulia mpaka ilipofika dakika ya 80, Ambapo timu hiyo ilirudi nyuma na kuanza kuzuia bao moja ambalo wamepata katika mchezo huo na Uganda wakishambulia kwa kasi ili kuweza kusawazisha.TanzaniaTimu ya Taifa ya Tanzania ilifanikiwa kuzuia bao lake moja mpaka dakika 90 zinamalizika na kufanikiwa kuondoka na alama zote tatu katika mchezo huo uliopigwa nchini Misri, Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa Machi 28 siku ya jumanne katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar-es-salaam.

Acha ujumbe