YANGA HAKUNA KULALA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, nguvu na hasira zake zote amezihamishia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara watakaocheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Hiyo ni baada ya kutoka kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama ya nchini Ghana, katika mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambao Yanga walikuwepo ugenini.YANGAYanga inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Desema 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Gamondi alisema kuwa wameuweka kando mchezo wao wa marudiano dhidi ya Medeama na sasa akili zao wanazielekeza mechi na Mtibwa Sugar ambao upo mbele yao.YANGAKocha wa Yanga Miguel Gamondi alisema kuwa anaamini kikubwa wanarejea katika ligi, kwa lengo moja pekee ambalo kushinda kila mchezo uliokuwepo mbele yao, kwa kuanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Acha ujumbe