Klabu ya Yanga imeungana na watani zao klabu ya Simba kuandika rekodi baada ya kufanikiwa kuongoza kundi kwenye kombe la shirikisho Afrika baada ya kufikisha jumla ya alama 13.
Yanga imefanikiwa kufikisha alama 13 kwenye kundi D kombe la shirikisho Afrika baada ya kuifunga klabu ya Tp Mazembe leo kwenye mchezo wa kumaliza hatua ya makundi, Rekodi hiyo klabu ya Simba walifanikiwa kuiweka msimu wa 2020/21 baada ya kuongoza kundi kwa alama 13 kwenye ligi ya mabingwa Afrika.
Klabu ya Yanga imefanikiwa kushinda michezo minne, Kufungwa mmoja na kutoka suluhu mchezo mmoja kwenye michezo sita waliyocheza hatua ya makundi, Hii ilifanywa na klabu ya Simba pia ambapo walishinda michezo minne, walifungwa mchezo mmoja na kusuluhu mmoja.
Wananchi mwaka huu wamekua na kiwango bora kwenye michuano ya Afrika baada ya kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho Afrika, Huku pia wakiwa na nafasi nzuri ya kumaliza kama vinara wa kundi lao jambo ambalo litakua zuri kwa upande wao.
Simba na Yanga ni klabu kongwe na zenye upinzani mkubwa katika ardhi ya Tanzania lakini mwaka huu zote zimefanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania baada ya kufuzu robo fainali ya michuano ya Afrika kwa pamoja, Simba akifuzu ligi ya mabingwa Afrika na Yanga wakifuzu kombe la shirikisho barani Afrika.

