Klabu ya Yanga imefanikiwa kuifunga klabu ya Tp Mazembe wakiwa ugenini kwa bao moja kwa bila na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC wakifanikiwa kumaliza mchezo wao wa mwisho kibabe.
Mchezo huo uliopigwa jijini Lubumbashi ilionekana mzani kua sawa kipindi cha kwanza timu ziote zikiwa zinashambuliana kwa vipindi, Lakini Tp Mazembe wakiwa wakionekana kuongoza kwa umiliki wa mpira zaidi lakini mchezo ulikwenda mapumziko bila kupatikana kwa bao lolote.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Tp Mazembe wakionekana kuja kwa kasi wakihitaji kupata bao la mapema zaidi kwenye mchezo huo, Lakini ni Yanga ambao walianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Farid Mussa ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Mudathir Abbas.
Kama klabu ya Us Monastir haitashinda mchezo wake hapo baadae au kushinda mabao yasiyozidi mawili klabu ya Yanga itafanikiwa kuongoza kundi D kwani mpaka sasa wameshafanikiwa kufikisha alama 13 wakiwa kinara wa kundi hilo mbele ya kwa alama tatu.
Yanga kama watafanikiwa kuongoza kundi lao watapata faida ya kukutana na timu iliyoshika nafasi ya pili katika kundi lingine ikiwa inaweza kua ahueni kwa upande wao, Mara nyingi inaaminika timu bora zinaongoza kundi na timu zinazoshika nafasi ya pili ubora wake hauwezi kua sawa na nafasi ya kwanza na ndio sababu inaweza kua faida kwa Wananchi.

