Klabu ya Yanga imetinga hatua ya robo fainali hapo jana kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuipasua US Monastir kwa mabao 2-0 na kuongoza kundi D kwa tofauti ya mabao ya kufunga.
Mabao hayo ya kuifanya Yanga iongoze kundi na iondoke na ushindi yalifungwa na Kennedy Musonda pamoja na Fiston Mayele katika vipindi vyote vya michezo huku kabla ya mchezo US Monastir ndiye alikuwa kinara wa kundi hilo.
Mechi ya kwanza Wananchi walipoteza walipokutana kule Tunisia kwa mabao hayo hayo mawili, hivyo jana wameweza kulipa kisasi chao na kuweza kutinga robo fainali wakiwa wamebakiza mchezo mmoja.
Mchezo huo watamenyana dhidi ya TP Mazembe ambayo ndio wanashikilia mkia katika kundi hilo baada ya kushinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo mitano aliyocheza.