Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu ‘Cadabra’, akisaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine akitokea Simba SC.

Ajibu amesaini mkataba jana Alhamisi mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi 2022.
Akizungumzia usajili huo, Popat amesema kuwa wamemsajili mchezaji huyo ili kuziba pengo la Salum Abubakar ‘Sure Boy’, aliyehamia katika klabu ya Yanga SC.
“Tumeondokewa na mchezaji wetu Sure Boy, timu haiwezi kwenda bila kuziba pengo lake tumekuwa na kocha anayekaimu (Abdihamid Moallin) katika mapendekezo yake ameonyesha anataka mbadala wa nafasi yake,” alisema.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

