Alex Telles Atimkia Al-Nassr

Klabu ya Manchester United imemuaga aliyekua beki wake raia wa Brazil Alex Telles ambaye ametumkia Saudia Arabia katika klabu ya Al-Nassr kwa uhamisho wa kudumu.

Klabu ya Manchester United imemuuza Alex Telles kwenda Al-Nassr baada ya kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo msimu uliomalizika ambapo aliitumikia klabu ya Sevilla na sasa anaondoka ndani ya klabu hiyo ambapo alijiunga mwaka 2020.Alex TellesBeki huyo wa kimataifa wa Brazil alijiunga na Man United mwaka 2020 ambapo alitua klabuni hapo kwajili ya kuimarisha upande wa kushoto pamoja na beki Luke Shaw, Lakini beki alipoteza namba kwa raia huyo wa kimataifa wa Uingereza na kumfanya kutolewa kwa mkopo.

Alex Telles anaungana gwiji Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr ambapo gwiji huyo alijiunga nayo mwaka huu mwezi Januari baada ya kutimka klabuni hapo na beki wa kimataifa wa Brazil na yeye ameunga tela.Alex TellesManchester United chini ya kocha Erik Ten Hag ina mpango mkubwa wa mbeleni na kwasasa inapitisha fagio la chuma kwa wachezaji wote ambao hawahitajiki ndani ya timu hiyo ili kujenga kikosi imara siku za usoni na miongoni mwachezaji hao Alex Telles alikua miongoni mwao.

Acha ujumbe