PSG wanata Euro Milioni 150 kwa Mbappe

Klabu ya PSG wameweka wazi kiasi cha pesa ambacho wanahitaji ili kumuachia mshambuliaji wao matata klabuni hapo Kylian Mbappe ambacho ni kiasi cha Euro milioni 150.

Klabu ya PSG wamewka wazi dau hilo ambalo kama kuna klabu itaweza kufikia basi itaweza kumpata Kylian Mbappe, kwani mabingw ahao wa Ufaransa ni wazi hawana mpango na mshambuliaji huyo kuelekea msimu ujao.psgMbappe aliondolewa kwenye kikosi cha klabu hiyo ambacho kitaelekea nchini Japan kwajili ya maandalizi ya msimu mpya, Hii ikionesha wazi kua mchezaji huyo hayupo kwenye mipango ya klabu hiyo kuelekea msimu wa 2023/24.

PSG wanasubiri ofa zije mezani kwa klabu ambayo itaweza kutoa kiasi cha Euro milioni 150 ambazo wao wanazitaka basi wataweza kumpata Kylian Mbappe ambaye kwasasa yupo sokoni huku klabu mlengwa zaidi ni Real Madrid.psgKylian Mbappe ameonekana akifanya mazoezi na wachezaji wa PSG ambao hawahitajiki kuelekea msimu ujao ambao ni Wijnaldum, Leandro Parades pamoja na Diallo hivo hii inaonesha wazi kabisa safari ya Mbappe ndani ya PSG imeiva.

 

Acha ujumbe