Andy Murray Aungana Tena na Ivan Lendl.

 

Mcheza Tennis wa Uingereza, Andy Murray na kocha Ivan Lendl wameungana tena kwa mara ya tatu huku wawili hao wakitarajiwa kufanya kazi pamoja kujiandaa na msimu mpya.

 

Lendl alifanya kazi kwa mara ya kwanza pamoja na Bingwa huyo wa US Open kuanzia mwishoni mwa 2011 hadi 2014 kwa ushirikiano wenye mafanikio.

Lendl alimuongoza Murray kutwaa taji lake la kwanza la Grand Slam kwenye US Open mwaka wa 2012 kabla ya mchezaji huyo kutwaa taji lake la kwanza la Wimbledon mwaka mmoja baadaye.

Lendl, mshindi mara nane wa Grand Slam, alirejea katika timu ya Andy mwaka wa 2016 alipomuongoza kutwaa taji lake la pili la Wimbledon na kuwa namba 1 la duniani kwa mara ya kwanza katika taaluma yake.

Walitengana kwa mara ya pili mwishoni mwa 2017, lakini baada ya miaka mitano, Bingwa namba moja wa zamani wa Czech ataanza tena kufanya kazi na Murray, 34 katika miezi michache ijayo.

Inafahamika kuwa watakaa pamoja kwa wiki kadhaa nchini Marekani baada ya Miami Open kwenye uwanja wa muda mrefu wa mazoezi, ambapo Murray na timu yake watajiandaa kwa msimu.

Murray, ambaye tayari amethibitisha kuwa atakosa msimu wa clay-court lakini amesisitiza azma yake ya kucheza Wimbledon, pia ana lengo la kuteua kocha wa ziada, ambaye atasafiri na kufanya kazi chini ya uongozi wa Lendl.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe