Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Ansu Fati ambaye amesajiliwa na klabu ya Brighton kwa mkopo amesema kocha wa klabu hiyo Roberto de Zerbi ana matumaini naye makubwa.
Ansu Fati ambaye amesajiliwa na klabu ya Brighton kwa mkopo wa msimu mzima anaamini ndani ya klabu hiyo anaweza kurejesha ubora wake ambao alikua nao ndani ya Barcelona kabla ya majeraha ya mara kwa mara kumuandama.Klabu ya Barcelona iliamua kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo kwajili ya kutunza kipaji chake, Kwani kocha Xavi aliona mchezaji huyo hatapata nafasi kubwa ya kucheza msimu huu ndani ya Barca na ndio sababu ya kumtoa kwa mkopo akapate nafasi ya kucheza zaidi.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Barcelona amesema kua kocha Roberto De Zerbi ndio alikua sababu kubwa ya yeye kujiunga na klabu ya Brighton na kuongeza kua kocha huyo amemuhakikishia kua anamuamini na kumfanya mchezaji muhimu kwenye timu hiyo.Mshambuliaji Ansu Fati amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ndani ya klabu ya Barcelona na kumfanya kupoteza nafasi kwani mchezaji huyo alianza vizuri ndani ya timu hiyo, Lakini anaamini kupitia Brighton anaweza kurejesha ubora wake.