Antony Arejea Mazoezini

Winga wa klabu ya Manchester United Antony Santos raia wa kimataifa wa Brazil amerejea mazoezini baada ya kupata majeraha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Real Betis.

Antony alishindwa kumaliza mchezo wa kirafiki dhidi ya Real Betis uliopigwa jana na kutolewa nje jambo ambalo lilizua taharuki kwa mashabiki wa Man United, Lakini mapema leo ameonekana katika uwanja wa mazoezi akijumuika na wachezaji wenzake hii ikionesha kua hakupata majeraha makubwa.antonyBaada ya kurejea kwa Antony mazoezini anayesubiriwa ni Marcus Rashford ambaye nae hakumaliza mchezo dhidi ya Real Betis uliopigwa jana kwasababu ya majeraha, Klabu ya Man United ni kama inaendelea ilipoishia msimu uliomalizika mabpo wachezaji wake waliandamwa na majeraha sana.

Manchester United kwasasa imebakiza wachezaji watatu ambao ni majeraha kati ya wanne walioumia kwenye kipindi cha kujiandaa na msimu mpya hiyo ni baada ya kurejea kwa winga wa Kibrazil, Leny Yoro, Rasmus Hojlund hawa wawili watakaa nje kwa muda kidogo huku Rashford ndio bado haijafahamika.

Acha ujumbe