Arsenal inaongoza Vita ya Kumuwania Rice

Klabu ya Arsenal inaongoza katika mbio za kumuwania nyota wa klabu ya West Ham United raia wa kimataifa wa Uingereza Declan Rice ambaye anatakiwa na vilabu vingi barani ulaya.

Klabu ya Arsenal kwasasa wanaonekana kua juu kuliko klabu yeyote katika vita ya kumuwania kiungo huyo na hiyo inaonekana ni wazi klabu hiyo inamuhitaji zaidi kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza, Washika mitutu wanamuhitaji Rice ili kuboresha safu yao ya ulinzi.arsenalDeclan Rice ambaye kwasasa ni nahodha ndani ya klabu ya West Ham amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu hiyo na amekua akifuatiliwa sana na vilabu mbalimbali nchini Uingereza kama Chelsea, Man United na hata klabu ya Liverpool wamewahi kuhushswa nae.

Klabu ya Arsenal watakumbana na changamoto ya dau ambalo watawekewa na klabu ya West Ham kwani inaelezwa dau la mchezaji huyo ni kubwa mno, Wiki kadhaa zilizopita kocha wa timu hiyo David Moyes alinukuliwa na kusema Rice atavunja rekodi ya usajili nchini Uingereza.arsenalKlabu ya Arsenal inatafuta mchezaji ambaye atakua anashirikiana na Thomas Partey kwenye eneo la kiungo wa ulinzi au kua mbadala kabisa, Kwani mchezaji huyo amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara hivo Rice akipatikana atakua mbadala mzuri wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana.

 

Acha ujumbe