Arteta: Tuna Mipango na Gabriel

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amesema kua beki wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Brazil Gabriel Magalhaes bado yupo kwenye mipango ya timu hiyo.

Beki Gabriel Magalhaes alikua anahusishwa na vilabu mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia, Lakini kocha Mikel Arteta amekanusha taarifa hizo na kusema moja ya wachezaji muhimu klabuni hapo ni beki huyo raia wa kimataifa wa Brazil.artetaBeki Gabriel amekua moja ya wachezaji muhimu klabuni hapo tangu ajiunge na timu hiyo na msimu uliomalizika alifanikiwa kucheza kwa kiwango bora sana ndani ya timu hiyo akishirikiana na William Saliba.

Beki huyo msimu huu ilionekana kama atakosa nafasi ndani ya timu hiyo baada ya kusajili kwa beki Jurien Timber, Lakini mchezaji huyo kwasasa anaweza kurudi kwenye nafasi yake baada ya beki Timber kupata majeraha ya muda mrefu.artetaKocha Mikel Arteta ameweka wazi kua nyota huyo ni mchezaji muhimu ndani ya timu hiyo na hamna chochote kinachoendelea juu ya tetesi za beki wake kutimkia Uarabuni na kutokana na kauli hiyo ni wazi beki huyo ataendelea kusalia klabuni hapo.

Acha ujumbe