Arthur Melo Kucheza Mechi ya Vijana Liverpool

Kiungo wa klabu ya Juventus anayekipiga ndani y klabu ya Liverpool Mbrazil Arthur Melo kukipiga katika mechi ya vijana wa Liverpool chini ya miaka 21 baada ya kutoka kwenye majeraha.

Kiungo Arthur Melo amekua akiandamwa na majeraha kwa kipindi kirefu tangu ajiunge na klabu ya Liverpool akitoka kwa mkopo klabu ya Juventus ya nchini Italia mwanzoni mwa msimu huu, Kiungo huyo sasa ni rasmi atakuwepo kwenye kikosi cha Liverpool kwenye michezo ijayo ya klabu hiyo.arthur meloKiungo huyo wa kimataifa wa Brazil alifanyiwa upasuaji mapema mwanzoni mwa msimu huu kutokana na tatizo lake la misuli ya paja ambalo limekua likimuandama, Lakini kwasasa anaendelea vizuri na ndio maana leo atacheza mchezo akiwa na timu ya vijana wa klabu ya Liverpool chini ya umri wa miaka 21.

Kiungo Arthur Melo anatarajiwa kujiunga na timu ya kwanza hivi karibuni baada ya kuonekana ameanza kukaaa sawa kutokana na majeraha ambayo yamekua yakimuandama mchezaji huyo toka ajiunge klabu hiyo akitokea klabu ya Juventus kwa mkopo wa msimu mzima.arthur meloArthur Melo amefanikiwa kucheza kwa dakika 13 tu tangu ajiunge na klabu ya Liverpool mwanzoni mwa msimu huu kutokana na majeraha ambayo amekua akiyapata mchezaji huyo, Hii inaonesha wazi kua kiungo huyo ametumia mda mrefu ndani ya Liverpool akiuguza majeraha kuliko kucheza.

Acha ujumbe