Klabu ya Real Madrid leo itashuka dimbani kuwaalika mahasimu wa klabu yaAtletico Madrid katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania utakaopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu.
Real Madrid leo watakwenda kuwaalika ndugu zao Atletico Madrid pale Santiago Bernabeu katika derby ya jiji la Madrid, Ambapo wenyeji wakiwa wanatafuta nafasi kutetea taji lao ambalo mpaka sasa kinara wa ligi hiyo klabu ya Barcelona wako juu.Atletico Madrid ambao wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya Hispania wao watakua wanatafuta namna ya kuhakikisha wanapa matokeo ili kuendelea kusogea juu na kujihakikishia nafasi ya kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa ulaya msimu unaofuata.
Real Madrid wao wamekua hawapo kwenye kiwango kizuri siku za karibuni katika ligi kuu ya Hispania, Lakini katikati ya wiki hii wamefanikiwa kupata matokeo mazuri dhidi ya Liverpool katika ligi ya mabingwa barani ulaya hivo inaweza kuwasaidia kuongeza morali yao kuelekea mchezo huu.Klabu ya Atletico Madrid wao wamekua wateja wa klabu ya Real Madrid katika siku za usoni na hata katika mchezo wa walipoteza walipokua nyumbani kwao, Hivo mchezo wa leo utakua mgumu kwakua vijana wa Simeone watakua wanahitaji kulipa kisasi.