Winga wa klabu ya Manchester Antony Santos amesema kua ushindi wa kombe la Carabao kesho dhidi ya klabu ya Newcastle unaweza kuirudisha klabu hiyo sehemu inapostahili kuwepo.
Klabu ya Manchester United kama itafanikiwa kubeba taji katika fainali ya kombe la Carabao hapo kesho dhidi ya klabu ya Newcastle United katika dimba la Wembley itaweza kufuta ukame wa miaka sita ambayo klabu hiyo imekaa bila kushinda taji lolote.Antony aliongea na tovuti ya klabu hiyo na kusema “Nilipokuja hapa nilisema kua Manchester United ni klabu kubwa na tutairudisha klabu hii inapostahili kwa kupambia na kushinda mataji, Tunajua itakua ngumu lakini tunafahamu sisi ni wakubwa kama klabu na jinsi tulivyo bora”
Antony aliendelea kwa kusema ” Itakua ndoto yangu imetimia kwa kuja hapa msimu wa kwanza na kushinda kombe, Natumai tutaendelea hivo na siku bora ziendelee” Winga huyo anaamini siku ya kesho ni siku ambayo inaweza kua ndo mwanzo sahihi wa kurejea kwa zama za mafanikio kwa klabu ya Manchester United.Klabu ya Manchester United haijafanikiwa kushinda taji lolote tangu mwaka 2017 ambapo walikua chini ya kocha Jose Mourinho baada ya hapo walifanikiwa kufuzu hatua ya fainali ya kombe la Europa League chini ya Ole Gunnar Solskjaer lakini hawakufanikiwa kushinda taji, Hivo ushindi wa kesho unaweza kuishiria mwanzo mpya wa mafanikio klabuni hapo.