Klabu ya Aston Villa leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Brighton and Hove Albion wakiwa ugenini katika dimba la American Express Community chini ya mkufunzi wao mpya Unai Emery.
Klabu hiyo ambayo imetoka kutolewa na klabu ya Manchester united kweny michuano ya Carabao katikati ya wiki baada ya kufungwa magoli manne kwa mawili na kutupwa nje kwenye michuano hiyo, Lakini wao wakitamba dhidi ya Man United kwenye mchezo ligi kuu wikiendi iliyopita.Klabu ya Aston Villa ilifanikiwa kuifunga Man United mabao matatu kwa moja wikiendi iliyomalizika wakiwa katika dimba lao la nyumbani Villa park, Leo wakiwa ugenini mtihani mkubwa kwa timu hiyo itakua ni kupata matokeo ugenini dhidi ya Brighton wanaoonekana kua vizuri sana msimu huu.
Baada ya kuja kwa mwalimu mpya klabuni hapo Unai Emery kuchukua mikoba ya Steven Gerrad klabu hiyo imeonekana kupata mwelekeo kwa kiwango fulani hasa kwenye ligi kuu ya Uingereza hivo mchezo wa leo unatarajiwa kua mgumu na wenye ushindani mkubwa.Aston Villa leo watawakosa nyota wao wawili waliopo kwenye majeraha ambao ni Philip Coutinho pamoja na Ollie Watkins ambae ameumwa ghafla, lakini kwa upande wa Brighton wao watakua kikosi kizima kwani hakuna huduma watakayoikosa kutoka kwa nyota wao yeyote.
Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.
BONYEZA HAPA