Aston Villa yafufuka Baada ya Gerrad Kutimuliwa.

Klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu Uingereza leo imefanikiwa kupata ushindi mnono katika ligi hiyo ambapo wamefanikiwa kuifunga klabu ya Brentford mabao manne kwa bila.aston villa Klabu ya Aston Villa imekua haipati matokeo ya kuridhisha katika michezo kadhaa ya ligi kuu Uingereza mpaka kupelekea klabu hiyo kumtimua aliekua kocha wake Steven Gerrard baada ya kupoteza mchezo katika ya wiki dhidi ya klabu ya Fulham.

Punde baada ya mwalimu Steven Gerrard kufukuzwa na mchezo wa kwanza klabu hiyo inaweza kuifunga klabu ya Brentford kwa jumla ya mabao manne kwa bila na hili kuonesha labda kweli kocha huyo ndio alikua tatizo klabuni hapo.Magoli yaliyoiwezesha klabu ya Aston Villa kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Brentford yalifungwa na Dany Ings akiweka mabao mawili kambani huku Ollie Watkins na mchezaji Leon Bailey ambao wamefunga bao moja kila mmoja.

Klabu hiyo kutoka mitaa ya Villa Park sasa imefanikiwa kushinda mchezo wake wa tatu kwenye michezo kumi na mbili na kufikisha jumla ya alama 12 hivo kuwafanya kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe