Aubameyang Aachwa Uingereza, Arsenal Ipo Dubai.

Hali ya sintofahamu inaendelea kwa Pierre – Emerick Aubameyang ndani ya kikosi cha Arsenal. Baada ya kuachwa kwenye kikosi, safari hii ameachwa tena.

Arsenal watatumia muda huu wa mapumziko kujifua zaidi kule Dubai. Kwa mara nyingine, Aubameyang sio sehemu ya kikosi cha timu hiyo kinachoenda huko. Hii inamaana gani?

Kwa hali ilivyo, Pierre alirejea Uingereza baada ya kusadikika kupata matatizo ya moyo akiwa na Timu ya Taifa ya Gabon kwenye mashindano ya AFCON. Kwa sababu za kiafya, ni kawaida wachezaji kurejeshwa kwenye vilabu vyao kwa uchunguzi zaidi.

Iliripotiwa kuwa mchezaji huyo anaendelea vizuri na anaimarika zaidi kurejea kwenye majukumu yake. Kabla ya AFCON, Pierre alivuliwa unahodha wa Arsenal na kwa muda sasa, amekuwa akifanya mazoezi peke yake, akitengwa na wachezaji wengine.

Ikumbukwe kuwa, Aubameyang anamkataba wa miaka 2 na Arsenal. Ripoti zinasema klabu hiyo inataka kumuuza kwenye dirisha hili la usajili ikiwa tayari klabu ya Al Nassr (ya Saudi Arabia) imeweka ofa ya kumsajili kwa mkopo utakoweza kubadilika na kuwa usajili wa moja kwa moja baadae.

Kama mchezaji, Pierre hana mpango wa kucheza soka kwenye falme za Kiarabu kwa sasa. Badala yake, ikitokea anaondoka Emirates majira haya, basi atajiunga na timu kubwa za Ulaya. PSG, Marseille na AC Milan zinahusishwa na mshambuliaji huyu.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe