Burudani ya mchezo wa tenesi inaendelea viwanjani. Stefano Tsitsipas ametinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi mnono.
Tsitsipas alikuwa uwanjani akichuana na Jannik Sinner katika mchezo wa robo fainali. Stefano yupo kwenye mchakato wa kulisaka taji lake la kwanza la Grand Slam katika maisha yake ya kucheza mchezo huu.
Mchezo uliodumu kwa masaa 2 na dakika 16, ulimshuhudia Stefano akiibuka kidedea kwenye seti zote (3) baada ya kupata matokeo ya seti 6-3 6-4 6-2 ndani ya uwanja wa Rod Laver Arena.

Mashindano ya Australian Open ya mwaka huu, ni nafasi kwa Stefano kufuta makosa aliyoyafanya kwa mwaka 2019 na 2021 ambapo, miaka hiyo yote alitolewa kwenye hatua hii hii (nusu fainali).
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.