Klabu ya Simba SC leo itashuka dimbani Kaitaba kuvaana na wenyeji Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi kuu ya NBC majira ya saa 10 kamili jioni.
Simba SC inaingia katika mchezo wa leo ikiwa imeshindwa kupata ushindi katika michezo mitatu iliyopita wakiambulia alama moja pekee kati ya sita, walipopoteza mbele ya Mbeya city na kutoka sare na Mtibwa sugar.
Kocha wa Simba SC, Pablo Franco, amesema mchezo utakuwa mzuri kutokana na uimara wa wapinzani pamoja na ubora wa uwanja ambao unaruhusu kuchezwa soka la aina yoyote.
“Mchezo utakuwa mzuri hata kuutazama sababu sehemu ya kuchezea ni nzuri kwa hiyo kila timu itakuwa na uwezo wa kucheza tofauti na mechi zetu zilizopita.
“Tunajua mechi itakuwa ngumu, Kagera ni timu nzuri inacheza soka safi na wapo kwenye kiwango bora sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Pablo.
Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.