Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Liverpool na Manchester City ndizo klabu zinazovutiwa zaidi kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na Ubelgiji Youri Tielemans, 24.

Tetesi zinasema, Ofa ya Tottenham ya takriban pauni milioni 38 kwa winga wa Porto kutoka Colombia Luis Diaz, 25 imekataliwa.

Aston Villa wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Juventus na Uruguay Rodrigo Bentancur, 24.

Newcastle haitamsajili mlinzi wa Brazil Diego Carlos kwani Sevilla wameamua kumbakisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28.

 

Liverpool

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 31, yuko tayari kuhamia Arsenal.

Juventus wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Dusan Vlahovic kutoka Fiorentina, na hivyo kuzima matumaini yoyote ya Arsenal kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 hadi Emirates.

Brighton wanamfuatilia kiungo wa Tottenham Dele Alli kwa nia ya kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini Burnley, Everton na Newcastle pia wanahusishwa na Mwingereza huyo.

Tetesi zinasema, Burnley wanakaribia kumsajili kiungo wa Dinamo Zagreb na Croatia Mislav Orsic, 29.

 

Arsenal Wanatemana na Dominic Calvert-Lewin?
Dominic Calvert-Lewin

Mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 24, kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves, 24, na Douglas Luiz wa Aston Villa, 23, wako kwenye orodha ya wanaowaniwa na meneja wa Arsenal Mikel Arteta.

West Ham wanafikiria kumnunua mlinzi wa Croatia na Marseille Duje Caleta-Car, wanatakiwa kulipa pauni milioni 20 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

AC Milan wanataka kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang. Mshambuliaji huyo wa Gabon mwenye umri wa miaka 32 anasemekana kukataa ofa ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe