Barcelona na Dembele Mazungumzo ya Mkataba Mpya Yavunjika.

 

Kulingana na jarida la michezo la Goal mkutano baina ya wawakilishi wa winga Ousmane Dembele na Barcelona umevunjika baada ya kushindwa kufikia makubaliano.

 

Kwa taarifa hizo sasa iko wazi Ousmane Dembele huenda akaondoka Barcelona msimu huu wa joto baada ya mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu hiyo kuvunjika.

Mazungumzo hayakwenda kama vile Barcelona walivyotarajia na maombi ya mkataba wa Dembele hayakutimizwa. Pande zinasalia mbali sana katika mapendekezo yao ya mishahara.

Hata hivyo, Meneja Xavi na uongozi wanasalia na matumaini kwamba makubaliano yanaweza kuafikiwa licha ya hali mbaya. Mkataba wa sasa wa Dembele unamalizika msimu huu na yuko huru kufanya mazungumzo ya awali ya mkataba na vilabu vingine kuanzia Januari 1.

Matumaini yalikuwa kwa Barcelona kufikia makubaliano na winga huyo wa Ufaransa kabla ya tarehe hiyo, lakini mazungumzo ya wiki hii yalivurugika pale Dembele alipokataa kukatwa mshahara.


KUWA MILIONEA MSIMU WA SIKUKUU NA SAHARA RICHIES

Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.