Kulingana na Jarida la Goal, Barcelona wanafikiria kumsajili Alex Sanchez kama mbadala wa Sergio Aguero baada ya kutangaza kustaafu soka hapo jana kutokana na matatizo ya moyo.

Barcelona wanamuangalia Sanchez kama mshambuliaji namba mbili wanaetaka kumsajili katika dirisha hili la usajili endapo watamkosa mshambuliaji wa Manchester City, Ferran Torres.
Taarifa zinasema endapo Barcelona watahitaji kumrejesha Sanchez pale Camp Nou kutoka Inter Milan, wanatakiwa kumjumuisha Luuk de Jong katika dili lolote watakalokubaliana.
Sanchez alicheza Barca kwa misimu mitatu, kuanzia 2011-2014 akifanikiwa kucheza mechi 141 katika mashindano yote na kufunga magoli 46 na kutoa pasi za magoli 27.
Akiwa Camp Nou sanchez ameisaidia kalbu hiyo kutwaa La Liga, Copa del Rey, Spanish Super Cup mara mbili pamoja na Club World Cup kabla ya kuondoka na kujiunga na Arsenal.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.


