Klabu ya Bayern Munich ambayo ipo chini ya kocha mkuu wake Julian Nagelsman yaendelea kupata sare mfululizo kwenye Bundesliga ambapo sare ya kwanza waliipata dhidi ya Borrusia Monchengladbach ambayo ilikuwa ya 1-1, ya pili ilikuwa dhidi ya Union Berlin, na ya tatu ikawa ni dhidi ya VfB Stuttgart.

 

Bayern Apata Sare ya 3 Mfululizo

Miamba hiyo ya Ujerumani ndani ya mechi tatu wamekuwa hawana ufanisi katika maeneno ya ushambuliaji na ulinzi kwani wamekuwa wakiruhusu magoli takribani kila mechi zao wanazocheza. Kati ya mechi sita ambazo amecheza mechi nne zote ameruhusu mabao.

Bayern japokuwa na kutoa sare hizo tatu mfululizo kwenye ligi bado wanaongoza ligi, huku akisubiri mchezo wa Freiburg wa leo kama asiposhinda atajihakikishia nafasi hiyo ya kwanza na kuangalia mechi zijazo anafanyaje. Freiburg ambaye ana alama sawa na Munich lakini akiwa yeye bado ana mchezo mmoja ambao anatarajia kuupiga leo dhidi ya Borrusia Monchengladbach.

 

Bayern Apata Sare ya 3 Mfululizo

Julian Nagelsman na vijana wake wanatarajia kuwakaribisha FC Barcelona siku ya Jumanne kwenye michuano ya klabu bingwa ambao utakuwa ni mchezo wake wa pili baada ya ushindi mnono alioupata dhidi ya Intermillan. Wakati kwa upande wa Barca nae ametoka kushinda mechi yake dhidi ya Viktoria Plizen. Mara ya mwisho kukutana timu hizi kwenye michuano hii Bayern alichukua alama sita zote huku akimpiga magoli sita pia kwenye mechi mbili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa