Presnel Kimpembe ambaye ni beki wa kati wa klabu ya PSG na timu ya Ufaransa yupo mbioni kukaa nje ya uwanja baada ya kuumia msuli wa paja katika mchezo wao wa nyumbani amabo walikuwa wakiwakaribisha Brest.

 

Kimpembe Aepuka Kadi Nyekundu

Kimpembe alinusurika kupata kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa timu ya Brest kitu ambacho kilifanya kocha wa timu hiyo Michel Der Zakarian kupatwa na hasira baada ya yeye kunusurika.

Beki huyo alinusurika, lakini aliondoka uwanjani akiwa ameshika msuli wake wa paja na kuwaacha wachezaji wenzake uwanjani wakiwa kumi bila kujali alipokuwa akitoka kwaajili ya matibabu huku wachezaji wote watano wa akiba tayari wameshatumika. Kutokana na kuumia huko inaonekana Kimpembe hatacheza dhidi ya Maccabi Haifa au Lyon kabla ya mapumziko ya kimataifa.

Kimpembe Aepuka Kadi Nyekundu

 

“Anauguza jeraha la misuli” Christophe Galtier alisema “Atakuwa na vipimo na tutasubiri ndani ya masaa 48 ili kuona makali”

Hata hivyo habari hizo hazikuwa nzuri kwa Der Zakaria baada ya golikipa Donnaruma kuokoa mkwaju wa penati uliopigwa na mchezaji wake kwani walikosa bao la kusawazisha na baadae mechi kumalizika kwa PSG kushinda bao hilo hilo 1-0 bao likifungwa na Neymar huku akipewa assist na Lionel Messi.

 

Kimpembe Aepuka Kadi Nyekundu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa