Waswahili husema ‘ chelewa chelewa utamkuta mwana sio wako’ Steven Bergwijn hataki kuchelewa wala kucheleweshwa tena. Spurs wamuachie?

Sekeseke la kutaka kuondoka Tottenham Hotspurs lilianza mwezi Januari lakini, uongozi wa klabu hiyo ulimgomea Steven Bergwijn kuondoka, hakuona tabu, alibaki kiroho safi. Kubaki kwake alitegemea angepata nafasi ya kuonesha uwezo wake uwanjani, Conte hakumpatia nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Steven mwenyewe, maisha ndani ya Spurs baada ya usajili wa Januari kukoma, yalikua magumu zaidi. Klabu haikumtazama kwa namna aliyoitarajia, hawezi tena kuendelea kuishi namna hiyo.

Bergwijn

Akiwa na timu ya Taifa ya Uholanzi kwa sasa, winga huyo ameonesha wazi dhamira yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo majira haya ya joto. Hataki tena kuwepo Spurs wakati timu hiyo haimpatii nafasi ya kucheza licha ya kuwa na kiwango kizuri kuzidi baadhi ya wachezaji wanaopewa nafasi na Antonio Conte.

Kwa Bergwijn, Ligi ya Mabingwa sio kigezo kikubwa kwake katika kuchagua timu anayoitaka. Anachokitaka yeye ni nafasi ya kucheza soka kila wiki na sio kuwekwa benchi au kutopewa nafasi kabisa.

Ajax ni timu inayohusishwa na mchezaji huyu kwa sasa, kwa uwazi aliouweka Steven akiwa na timu ya Taifa, huenda vilabu vingine vikajitokeza na kujaribu kuweka ofa mezani ili kumsajili winga huyu mwenye umri wa miaka 24.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa