Botman Anawatoa Nishai Wanaomuhitaji.

Beki kisiki wa Lille, Sven Botman, anavichachafya vilabu vinavyowania sahihi yake. Kuna kazi ya ziada kumtoa Ufaransa.

Newcastle United na AC Milan ni vilabu viwili vinavyohusishwa zaidi na Botman katika dirisha hili la usajili. Kwa hali ilivyo, Lille wanaweka ugumu kwa usajili huu kufanyika. Milan wameanza kuamini kuwa, huu ni mpango wa Lille kutotaka kuachana na mchezaji huyo ambaye amewekewa thamani ya £41M.

Inasemekana, Milan wameamua kujiondoa kwenye mchakato wa kumsajili beki huyu na, badala yake, viongozi wa Milan wanahamishia majeshi kwenye timu ya PSG wakimsaka Abdou Diallo.

Hata Diallo hatopatikana kirahisi, PSG wameweka thamani ya £16.7M. Milan wanataka kutumia mfumo waliotumia kumtoa Fikayo Tomori kule Stamford Bridge. Wanamuhitaji Diallo kwa mkataba wa mkopo ambao utakuwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu.

Kwa Botman, wamebaki Newcastle United pekee. Watafanikiwa kumtoa Lille au wataamua kuchukua uamuzi kama wa AC Milan?


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.